Kirjojen hintavertailu. Mukana 12 452 910 kirjaa ja 12 kauppaa.

Kirjahaku

Etsi kirjoja tekijän nimen, kirjan nimen tai ISBN:n perusteella.

8 kirjaa tekijältä Mohammed Ghassani

N'Na Kwetu

N'Na Kwetu

Mohammed Ghassani

Lulu Press Inc
2021
pokkari
DIWANI hii ya N'na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini ilishinda kwenye awamu ya kwanza ya Tuzo za Fasihi ya Afrika kwa Lugha ya Kiswahili inayotolewa na Wakfu wa Mabati-Cornell mwaka 2015. Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kujitambulisha nayo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa " Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.
Siwachi Kusema

Siwachi Kusema

Mohammed Ghassani

Lulu Press Inc
2021
pokkari
SIWACHI KUSEMA: Uhuru U Kifungoni ni diwani ya pili kuchapishwa na mshairi wa Kiswahili, Mohammed Khelef Ghassani, aliyezaliwa na kukulia Zanzibar na ambaye anaishi na kufanya kazi nchini Ujerumani.
Andamo

Andamo

Mohammed Ghassani

Lulu Press Inc
2021
pokkari
ANDAMO: Msafiri Safarini ni diwani ya kwanza kuchapishwa na mshairi wa Kiswahili, Mohammed Khelef Ghassani, mzawa wa Zanzibar anayeishi na kufanya kazi nchini Ujerumani. Ndani yake ni muakisiko wa safari yake ya ukuwaji baina ya muongo wa mwisho wa 1990 na muongo wa kwanza wa 2000. Kuisoma diwani hii ni kuyasoma maisha yake na yale yaliyomuandama, naye kuyaandama katika umri huo.
Simulizi Za Bi Time

Simulizi Za Bi Time

Mohammed Ghassani

Lulu Press Inc
2021
pokkari
Huu ni mkusanyiko wa hadithi za paukwa-pakawa zinazosimuliwa katika jamii za Waswahili wa visiwa vya Zanzibar kama ambavyo mwandishi anazikumbuka. Huenda usimulizi wa upande mmoja wa jamii ya Waswahili ukatafautiana na wa jamii nyengine, lakini kwa kuwa wenyewe husema "Hadithi ina ncha saba", basi hii ni moja kati ya ncha hizo.